ZABURI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD



ZABURI YA SHEREHE ZA MIAKA 75 YA UWEPO WA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD (TAG)

1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

2 Mshukuruni Mungu wa miungu
    Kwa maana fadhili zake ni za milele

3 Mshukuruni Bwana wa Mabwana
    Kwa maana fadhili zake ni za milele

4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

5 Alimtuma Paul Derr toka Marekani hata Igale
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

6 Akamtumia kuwasha moto mkuu wa uamsho Igale
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

7 Watu kwa mamia wakaokolewa, wakaponywa, na kujazwa Roho Mtakatifu
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

8 Akajichagulia Yohana Mpayo na Moses Kametta, baadhi ya watumishi wake
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

9 Akawatia nguvu wakasafiri maili 120 hadi Malawi kwa miguu
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

10 Wakataka ushirikiano wa huduma toka kwa Wamisioni waliokuwa Malawi
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

11 Akawapa kibali machoni mwa Wamisioni wa Assemblies of God wakaja kuwalea
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

12 Wamisionary wakawa nguzo ya kulitegemezana kulikuza Kanisa
    Kwa maana fadhili zake ni za milele

13 Wakajenga misingi ya elimu ya kiroho kwa kuanza Vyuo vya Biblia
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

14 Moto wa uamsho ukawaka Itende hata madarasa yakageuka “Azusa”
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

15 Arusha Bible College ikawasha moto Kaskazini, Dodoma na Mwanza
    Kwa maana fadhili zake ni za milele


16 Walisuka Kanisa kwa Idara za CA”s WWK, Sunday School na Machapisho
      Kwa maana fadhili zake ni za milele

17 Idara zikawa nguzo za Kanisa katika kukua kwake
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

18 Alilitia Kanisa katika usimamizi wa Watumishi wenyeji wa Tanzania
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

19 Akajiinulia Watumishi wa kuliongoza Kankisa kwa awamu akiwapa majukumu
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

20 Akampa Lazaro kukoleza uamsho nchi nzima
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

21 Akamuwezesha kulivusha Kanisa katika kipindi hatari cha mgawanyiko
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

22 Akamuinua Mwenisongole apokee kijiti kwa Lazaro
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

23 Akamtumia kuongoza ujenzi wa Makao Mkuu na Elimu ya Watumishi
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

24 Alimuinua Mtokambali apokee kijiti cha uamsho
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

25 Akamtumia kuliongoza Kanisa kimkakati
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

26 Kanisa likakua kama uyoga pande zote hata ulimwengu ukazizima
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

27 Ametujalia kufikia miaka 75 ya uwepo wa Kanisa
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

28 Alituma wimbi la uinjilisti nchi nzima, nchi ikavunwa kama ngano
     Kwa maana fadhili zake ni za milele

29 Akatupa amani na utulivuTanzania kipindi chote cha Kanisa hadi leo
   Kwa maana fadhili zake ni za milele

30 Mshukuruni, Msifuni, Mwabuduni kwa Ukuu wake
    Kwa maana fadhili zake ni za milele

ZABURI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD ZABURI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD Reviewed by Unknown on 2:56 PM Rating: 5

No comments:

ads
Powered by Blogger.