Tanzania Assemblies of God Ilianza lini hapa Tanzania

LINI KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD LILIANZA HAPA TANZANIA??

Miaka 75 ya Tanzania Assemblies of God - TAG

KWA UFUPI, Mmishonari Paul Deer aliingia nchini na kuanzisha  kazi ya Mungu  mwaka 1928 kama mmishenari binafsi. Takwimu za kihistoria zinatuonesha kuwa mtumishi huyu aliikabidhi huduma yake aliyoainzisha Tanganyika  kwa Assemblies of God (AG) kule Marekani  mwaka 1939. Hapo ndipo hesabu za umri wa kanisa letu  hapa nchini zinapoanzia, hivyo kutupa uhalali wa kusherehekea miaka 75,  ya uhai wa  Tanzania Assemblies of God Mwaka huu wa 2014.

Historia inatuonesha kuwa katika miaka ya mwanzo  kanisa lilisimamiwa  wamishenari wa  kimarekani, wachungaji wa kiafrika  wakati huo, Yohana Mpayo (Marehemu) na  Petros, walikuwa maaskofu  chini ya Assemblies of God Mission. Kanisa liliendelea kuongozwa katika mfumo huo hadi mwaka 1967. Kanisa la kwanza kabisa la TAG lilikuwapo pale Igale, Wilaya ya Mbalizi, Mkoa wa Mbeya.

Ni mwaka huo wa 1967, uongozi wa Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa wenyeji na Mchungaji Immanuel Lazaro, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mtanzania wa  kuongza Tanzania Assemblies of God (TAG).

Kanisa hili liiingia hapa nchini kama matokeo ya uamsho mkubwa wa Kipentekoste uliotokea kule Azuza Marekani. Hivyo lengo kuu la kuanzishwa kwa kanisa ni kuwafikia wenye dhambi kwa injili iliyo hai, iletayo wokovu na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo hapa nchini. ili kutimiza lengo hilo ilikuwa lazima watendakazi shambani mwa bwana waandaliwe tangu utoto wao.

KWA MAELEZO ZAIDI PATA NAKALA YA KITABU CHA HISTORIA YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, pale makao makuu ya TAG, Ubungo.
Tanzania Assemblies of God Ilianza lini hapa Tanzania Tanzania Assemblies of God Ilianza lini hapa Tanzania Reviewed by Unknown on 3:20 PM Rating: 5

5 comments:

  1. Naomba kupata kitabu Cha Historia ya kanisa la T .A.G 0717519843. Mnitafute

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda Sana hiyoo historia ya kanisa letu zuri la tag

    ReplyDelete
  3. Nimeipenda historia ya kanisa letu zuri la TAG

    ReplyDelete
  4. Kwa hapa Tanzania nani aliazisha TAG

    ReplyDelete

ads
Powered by Blogger.