Askofu Mkuu Wa Tanzania Assemblies of God

Rev. Dr. Barnabas Mtokambali
Rev. Dr. Barnabas Mtokambali
Dr Barnabas Mtokambali ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Bethel Revival Temple, Mtaa wa Mwembe Songo, Morogoro Mjini, Katika mkoa wa Morogoro, Tanzania

Kwa mara ya Kwanza Dr. Barnabas Mtokambali alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa TAG kwa kipindi cha miaka 4 (minne 2009 - 2012) katika Mkutano mkuu wa Mwaka 2011.

Kwa awamu nyingine ya pili Dr Barnabas Mtokambali alichaguliwa kuwa askofu wa TAG kwa kipindi cha miaka minne (2013-2016)
Rev. Dr. Barnabas Mtokambali atoa machozi Baada ya Kuchaguliwa kushika nafasi ya Uaskofu kwa awamu ya Pili
Aibuka na ushindi wa theluthi mbili ya kura zote
Wachungaji asilimia 93 kati ya 2717 waliopiga kura Katika Uchaguzi Mkuu Wa Tanzania Assemblies Of God Wamemrejesha Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr. Barnabas Mtokambali katika Nafasi yake ya Uaskofu. Dr. Mtokambali amepata ushindi huo wa Kishindo baada ya kupendekezwa na wajumbe kugombea tena nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo hayo Mmisionari Gregorry Beggs, kutoka USA, alimtangaza Askofu Dk. Mtokambali kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo kwa awamu nyingine  baada ya kupata theluthi mbli ya kura zote zilizopigwa wakati wa mapendekezo ya majina ya wagombea, ambapo idadi ya wapiga kura wote waliokuwa ni 2717, na Dk. Mtokambali alipata kura 1969, kati ya kura 2116 zilizopigwa sawa na asilimia 93
Makamu Askofu Dr M Mhiche (kushoto) Askofu mkuu Dr B Mtokambali (katikati) Katibu Mkuu Rev R Swai (kulia)

Arudi madarakani  na timu yake yote iliyochaguliwa katika mkutano mkuu wa mwaka 2008.


Askofu Mkuu Wa Tanzania Assemblies of God Askofu Mkuu Wa Tanzania Assemblies of God Reviewed by Unknown on 6:37 PM Rating: 5

1 comment:

  1. “nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu.

    — Yeremia 3:15 (Biblia Takatifu).

    Ahadi ya BWANA

    ReplyDelete

ads
Powered by Blogger.