Wednesday, November 2, 2016

Ambassadors Mega Festival - MEGAFEST


Conference kuubwaa ya vijana  
(Ambassadors Mega Festival) 

Hii ni zaidi ya kambi zaidi ya mkutano zaidi ya Fiesta na zaidi ya sherehe
Hizi shamrashamra zitahusisha

 • Vijana wote chipukizi (Teenagers) - chini ya Miaka kama 19
 • Vijana zaidi ya miaka 19
 • Waalimu na Wasimamizi
Wahusika ni Watu wote:

Idara zote za watoto na Chipukizi
Idara zote za Vijana
Idara zote za Wanafunzi -Secondari, Vyuo na Vyuo vikuu
Waalimu na wasimamizi mbalimbali wa watoto na vijana
Wadau wote wa watoto na vijana
Watu wote mnakaribishwa.Itafanyika tar 7 hadi 12 Novemba 2016
Mahali -  kambi kuu ni Chuo Kiku cha Dodoma - UDOM 


***Tarehe 11 November - MEGA NIGHT***
============================= 
(Fiesta ya Mkesha, burudani nk) 
hadi kunakucha

Mahali - Uwanja wa Jamuhuri - Dodoma


Ada 
Tsh. 25,000/= 
Vijana chipukizi(teenagers) na walimu wa vikundi vitakavyokuja

Tsh. 30,000/=  
Vijana wengine wenye umri zaidi ya teenagers ada ni


Kufika
7/11/2016 - Vijana wote wakubwa
8/11/2016 - Watoto na Chipukizi (Teenagers)

Mafundisho mazuri sana yatakuwepo pamoja na ibada kubwaa za kusifu na kuabudu. Watoto kuanzia umri wa teenager na vijana msikose kufika. Pia waalimu wa watoto tunawakaribisha Saana! Kutakuwa na wanenaji na waimbaji wengi maarufu.


Don't plan to miss

Tuesday, August 12, 2014

100 Years Assemblies of God US Cerebration


Askofu mkuu Barnabas Mtokambali,
Katibu mkuu Ron Swai,
Askofu wa jimbo la Zanzibar Mch Kaganga,
Wakifanya presentation USA ktk Mkutano Mkuu wa dunia unaoitwa GLOBAL CHURCH PLANTING SUMMIT. Kuonesha kwa mfano jinsi Tanzania tulivyofanikiwa ktk Kitengo hicho cha kupanda makanisa ( Church Planting)

Barnabas Mtokambali 100 years US Assemblies of God from Godfrey Kitangala on Vimeo. FOR MORE INFORMATION ABOUT 

IF YOU WANT TO SEE MORE ABOUT US ASSEMBLIES OF GOD 100TH YEAR CEREBRATION CLICK BELOW

100 THE CENTRAL ASSEMBLIES OF GOD


GOD IS GOOD ALL THE TIME

Tuesday, July 1, 2014

RATIBA MTIRIRIKO WA MATUKIO WIKI YA JUBILEE YA TAGMTIRIRIKO WA MATUKIO WIKI YA JUBILEE
TAREHE
TUKIO
WAHUSIKA
 1 July 2014
·        Kufika Mbeya
·        Kuzindua Kampeni ya Huduma kwa Jamii
·        Kamati ya Utendaji
·        Askofu Mkuu
·        Mkuu wa Mkoa – Mbeya

2-4 July 2014
·        Kusambaza  Vyandarua vya Mbu Mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa
·        Kamati ya Utendaji
·        Kamati za Majimbo husika
·        Kamati ya Huduma kwa Jamii
5 July 2014
·        Kuzindua Radio Ushindi
·        Kamati Husika
7 July 2014
·        Kuzindua Jengo la Kanisa Igale
·        Wajumbe wa Halmashauli Kuu Kufika
·        Wahusika wote
8 July 2014
·        Kikao Cha Halmashauli kuu ya TAG Mbeya
·        Wajumbe wa Halmashauli Kuu
9 July 2014
·        Kikao cha Halmashauli Kuu
·        Kuzindua Chuo cha Kupanda Makanisa Jimbo la Kusini Magharibi
·        Wahusika
10 July 2014
·        Baraza la Waangalizi
·        Kufika Wajumbe wa Mkutano Mkuu/ Baraza Kuu
·        Baraza
11 July 2014
·        Mkutano Mkuu/ Baraza Kuu
·        Kusimika Wainjilisti
·        Wahusika
12 July 2014
·        Mkutano Mkuu
·        Kusimika Wachungaji
·        Wahusika
13 July 2014
·        KILELE CHA JUBILEE
·        WOTE


Thursday, June 19, 2014

WALIOCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO KWA MWAKA 2014/2014

 KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD LINAPENDA KUWAPONGEZA VIJANA WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA HUU WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG

HAYA NDIYO MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2014/2015

Wasichana Wote ====> herufi A mpaka Z  

bonyeza hapa kusoma na KUDOWNLOAD 
Kama unashindwa kutazama kwa link hiyo hapo juu basi Tazama hapa

Wavulana ===>herufi A mpaka L

   Bonyeza hapa kusoma na KUDOWNLOAD
Wavulana ===>herufi M mpaka Z
Bonyeza Hapa kusoma na Kudownload 
Kama unatumia simu na hapo juu unashindwa kutazama basi Tazama hapa
 

Sherehekea Jubilee ya Miaka 75 ya TAG Live

Sherehekea Jubilei ya miaka 75 ya TAG  Live!

Tukio la kihistori la maadhimisho ya miaka 75 ya kanisa la TAG litakalo ambatana na Mkutano wa Injili wa Kimataifa Utakaohubiriwa na Rev Johannes Amritzer - Sweeden, litaoneshwa  moja kwa moja (Live) kutoka uwanja wa Sokoine Mbeya, na vituo vya Television ATN na Fire TV,  Julai 13 mwaka huu 2014
Ni tukio la aina yake litakalokusanya wageni  zaidi ya 10,000 kutoka mataifa mbali mbali. Wakiongozwa na Mgeni rasmi  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa makanisa ya Assemblies of God (AG) Duniani, Dk. George Wood, na maaskofu kutoka mataifa mbali mbali.
Wasioweza Kufika Mbeya wanaweza kuungana na Maelfu ya wenzao uwanjani wakiwa Makanisani, Section, Jimbo au hata sebuleni kwao Kushuhudia tukio hilo.
Usichelewe!  Nunua King’amuzi chako cha TING (Tanzania Integrated Network Group), sasa kutoka katika vituo vya mauzo vilivyotajwa hapo chini kabla havijaisha maana vimebaki vichache.
Kumbuka king’amuzi hiki ni cha teknolojia ya kisasa zaidi ya  vyote High Definition Quality  (HD) Inayokupa nafasi ya kurekodi vipindi ukaangalia baadaye.
 
GHARAMA: Kunaving'amuzi aina mbili
 • King’amuzi cha antenna za Kawaida, kitakachokupa mtandao makini katika mikoa ya: Dar,  Arusha, Dodoma, Mbeya, Sumbawanga, Mwanza, Kigoma, na  Tanga. (Coming soon to Songea)  Bei yake ni Tsh 76,000/ + Miezi 2 ya kwanza kutumia bure 
 • Kingamuzi cha TING kinachotumia  Satellite bila chenga wala mikwaruzo Kinakupa zaidi ya chanel 100 Kinaonekana bara zima la Afrika.
  Bei yake ni Tsh: 176,000 TU + Miezi 2 ya kwanza kutumia bure

  Uongozi wa TAG makao makuu unawahimiza wakristo wote wa TAG, makanisa  na wote wenye mapenzi mema kununua ving’amuzi hivyo ili kushuhudia moja kwa moja tukio hilo la kihistoria.
Unaweza kupata king’amuzi chako katika vituo vya:
Makao makuu ATN ,  Mbezi Beach: 0653/0767/0684 999 230
Mwenge: 0659 970 860
Temeke: 0659 970 865
Victoria: 0659 970 861
Tabata: 0715 572 825
Mbezi Kimara: 0716 145 556
Arusha: 0658 387 036
Dodoma: 0658 387 024
Mwanza: 0658 387 021
Mbeya: 0658 387 039
Tanga: 0658 387 034
Kigoma: 0752 512 300
mawakala:
Dar es Salaam:
Maranatha: 0754 204 098
Bale Investment: 0713 799 382
Kumbe Traders Ukonga: 0657 544 954
Rich Electronics Mbagala: 0652 446 790
Kibaha Maili Moja: 0766 666 999
Mmas Kariako 0755 867 758
Nesto Sinza: 0758 053 723
Arusha Agents:
Mwanga Shop: 0754 822 313
CCM Mkoa: 0754 373 380
Mbeya s:
Genesis Electronics: 0655 493 874
Kisimpya S. Power: 0755 149 216
Maranatha: 0768 340 047
Dodoma s:
City Boys: 0715 816 313
Sumbawanga : 
Stendikuuu: 0754 822 313
Mwanza:  Electronics Mwanza Mjini
Bukoba: 0754 306 497
Morogoro: 0713 978 597
Tabora: 0786 409 456
Singida: 0759 330 859
Shinyanga: 0713 377 398
Iringa: 0757 800 210
Katavi: 0655 530 020
Sumbawanga: 0767 907 795
Songea: 0717 084 799
Usisubiri majuto nunua sasa king’amuzi chako

Idara ya Elimu washerekea Maadhimisho ya Miaka 75 ya TAG

MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA TAG IDARA YA ELIMU KATIKA PICHA
Idara ya Elimu,
Idara hii ambayo kwa sasa makao yake Makuu yapo Dar es Salaam Ubungo, Inayosimamia vyuo vya biblia zaidi ya 6 vikubwa kwa sasa (Dodoma, Mwanza, Mbeya, Arusha, Mtama, Dar es Salaam) Walifanya sherehe ya Jubilee ya Miaka 75 tangu Assemblies of God pale Mjini Dodoma
Sherehe hizo ziliambatana na
 1. Maandamano
 2. Kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Dodoma inayotwa General Hospital Dodoma
 3. Kutoa Misaada vitu na Vyakula katika Hospitali ya Dodoma 
 4. Kuwahubiria Wagonjwa 
 5. Kuwaombea wagonjwa
 6. Kufanya Mkutano Wa Injili

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God


Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Idara ya Elimu ya Tanzania Assemblies of God

Tuesday, June 17, 2014

Mpango Mkakati wa TAG Miaka 10 ya Mavuno - Tanzania kwa YesuTANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

TAMKO LA KUJIWEKA WAKFU KWA AJILI YA MIAKA 10 YA MAVUNO – TANZANIA

(DECADE OF HARVEST TANZANIA 2009 – 2018)

Kwa kuwa TUNAAMNI katika Agizo Kuu ambalo linatutuma kuhubiri habari njema ulimwenguni kote na kwa kila kiumbe (Mathayo 28:19); Kwa kuwa TUNAAMINI kuwa sasa ni wakati wa mavuno kwa taifa la Tanzania; Kwa kuwa TUNAAMINI kuwa tamko la Halmashauri Kuu lilipitishwa na Baraza la Waangalizi na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu (Kupitia Conference za Majimbo yote kumi). Kwamba miaka hii kumi ya 2009-2018, kuwa ni miaka kumi ya mavuno. Tukiwa tumeisikia vema sauti ya Roho Mtakatifu akiongea na mioyo yetu kama watumishi viongozi tuliojitoa kikamilifu na wenye maono makubwa. Sisi Kanisa la Tanzania Assemblies of God, tunatamka tamko la kujiweka WAKFU kwa Bwana na UWEZA wa NGUVU ZAKE kama ifuatavyo:-

TUNAJIWEKA WAKFU kufunga na kuomba na kuendelea, na kuhubiri mahubiri ya Kipentekoste tukitazamia umwagiko wa Roho Mtakatifu katika nchi yote ya Tanzania. Tukiomba sawasawa na 2Nyakati 7:14; kwa ajiil ya uamsho mkuu Tanzania unaoambatana na nguvu za Kipentekoste, mahubiri yenye nguvu na udhihirisho na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kwa kiwango kamili katika kanisa lake (Mdo. 1:8).

TUNAJIWEKA WAKFU SISI WENYEWE kwa makusudi kabisa kumfikia kila mtu katika Tanzania kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya na Miji yote kwa ushuhuda wa Injili kamili (Yesu anaokoa, Yesu anaponya, Yesu anajaza Roho Mtakatifu na Yesu anarudi tena). Ili lengo hili lifanikiwe, tutatumia kila mbinu ya kuhubiri; Radio, Televisheni, Maandiko, Tovuti, Mtu kwa Mtu, Michezo, Mikutano, huduma maalumu na vyanzo vingine halali. Tunaunganisha nguvu zetu katika taifa zima kama kanisa, pamoja na washirika wenza ndani na nje ya nchi, watakaosimama nasi katika kuvuna mavuno haya na kuyaleta ghalani.

TUNATHIBITISHA KUJIWEKA KWETU WAKFU kwa kuanzisha makanisa imara, kuwafunza na kuwawezesha wote ambao Bwana anawaita katika mavuno haya. Kwa hiyo tumeazimia kuimarisha huduma ya kanisa inayoweza kufanya umisheni katika maeneo yasiyofikiwa ndani na nje ya mipaka ya nchi.

TUNAWAITA WATUMISHI WOTE wa TAG waanzishe maombi na maombezi ya kipekee kwa ajili ya miaka 10 ya mavuno.

TUNAWAITA watumishi wote wa TAG waonyeshe uhai mpya na maono mapana ya kimisheni ikiambatana na kupeleka watumishi maeneo yasiyofikiwa ili Yesu Kristo ahubiriwe kwa kila mtu. TUNATANGAZA vita vya kiroho katika nchi nzima, tukishambulia wakuu na nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho kama itamkwavyo katika Waefeso 6:12; tukijua ya kwamba sisi ni WASHINDI NA ZAIDI YA KUSHINDA kwa Yeye aliyetupenda (Rum 8:12).

TUNAAMINI kwa uweza wa Mungu tutatenda MAKUU hadi kufikia malengo yafuatayo: -

Ø  TUNAMWAMINI MUNGU KUWA NA UAMSHO utakaomwagika nchi nzima na kusababisha mafuriko makubwa ya utendaji wa Roho Mtakatifu kwa kanisa kama matokeo ya kujiweka wakfu na kuomba kusikokoma kwa washirika wote.
Ø  TUNAMWAMINI MUNGU KUWA NA WASHIRIKA 2,000,000 ifikapo mwaka 2018. Hii ina maana kila mshirika ni mtenda kazi kwa hiyo amlete mwongofu mpya mmoja au zaidi kila mwaka.
Ø  TUNAMWAMINI MUNGU KUWA NA MAKANISA 10,000 ifikapo mwaka 2018. Kila kanisa lizae kanisa moja au zaidi kila miaka mitatu.
Ø  TUNAMWAMINI MUNGU KUWA NA WACHUNGAJI 10,000 ifikapo 2018. Kila Mchungaji aliyepo azae mchungaji mmoja au zaidi na kuwawezesha kusoma chuo cha utumishi.
Ø  TUNAMWAMINI MUNGU KWAMBA KILA JIMBO LITAKUWA NA CHUO CHA KUPANDA MAKANISA, pia kuviongeza, kuvipanua na kuviboresha vyuo vyote vilivyopo kwa lengo la kuharakisha kasi ya kuvuna na kutunza mavuno.
Ø  TUNAMWAMINI MUNGU KUWA, katika kanisa kuwajibika kwa jamii kila Jimbo na Idara itaanzisha au shule ya chekechea ama msingi au sekondari ama vyote kwa pamoja.
Ø  TUNAMWAMINI MUNGU kufanya zaidi ya yale tunayoweza kufikiri na kuwaza huku tukiendelea kukusanya mavuno kwa uaminifu.

KWA KUTEKELEZA HAYO:
·         Neno la Mungu litakuwa mwongozo wetu na mpango wetu wa kazi
·         Kweli za Kibiblia zisizoyumbishwa, zisizopunguzwa zitakuwa jumbe zetu za Injili
·         Roho wa Mungu atakuwa mwezeshaji na nguvu Yetu ya huduma
·         Damu ya Bwana Yesu Kristo inatuhakikisha ushindi.
·         Kanisa litakuwa kiroho, kiidadi, kijiografia, kiufanisi, na kwa wana wapotevu kurudi kwa Bwana Yesu.

KAULI MBIU YETU: MIAKA KUMI YA MAVUNOOO!!! TANZANIA KWA YESU.
TANZANIA KWA YESUUU!!! MIAKA KUMI YA MAVUNO.