UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG

UZINDUZI WA SHEREHE ZA JUBILEE PALE MBALIZI TAREHE 18, JANUARI 2014

Mwaka 2014 Tanzania Assemblies of God Inasherekea Miaka 75 Tangu kanisa hili lianze hapa Tanzania Mwaka ule wa 1939 Pale Igale, Wilaya ya Malizi, Mkoani Mbeya. Kanisa hili likikuwa linasimamiwa na Wamishonari kwa Mda huo. Huo mwaka 1939 ndio mwaka ambao kanisa lilikabidhiwa Makao Makuu ya Assemblies of God Marekani.
Uzinduzi wa Maadhimisho ya Tanzania Assemblies of God TAG





  •  
  • KWANINI TUNASHEREHEKEA MAADHIMISHO??
Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God Rev Dr Barnabas Mtokambali alizungumzia theology ya sherehe za maadhimisho ktk Biblia kitabu cha Kumb 16:1-17. Wakristo wengi sasa sio watu wa maadhimisho sana ndio maana ukifika wakati wa maadhimisho wanakosea kiasi kwamba tusipokuwa waangalifu itafika mda sherehe za Kikristo zitakuwa mapokeo tu, kitu ambacho Mungu hakimpendezi. Askofu mkuu alisema Maadhimisho ambayo Mungu anapenda ni yale ambayo YANAFANYA IBADA NA SHUKRANI KWA MUNGU

Ona sasa sherehe mfano HARUSI, SEND OFF, KITCHEN PARTY, BEG PARTY na Anniversary mbalimbali zinavyofanyika, Nyingi zimejaa anasa, kula na kunywa na kucheza tu, na nyingine zimeingiza na mambo ya kidunia ndani yake. IBADA hakuna, hata kama zipo ni kidogo tu kutimiza sheria kuonesha hiyo niibada ya wakristo. Fedha nyingi zinazochangwa zinatolewa kwaajili ya kula na kunywa na si Kumshukuru Mungu/Sadaka ya shukrani, hata kama ipo ni kidogo. MUNGU ANAPENDA TUNAPOSHEREKEA TUMSHUKURU NA KUMFANYIA YEYE IBADA

SHEREHE HIZI ZA JUBILEE ZA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD si kula na kunywa na anasa. NI SHEREHE ZA KUMSHUKURU NA KUMUOMBA MUNGU. Hivyo sherehe zote zinazofanyika ktk ngazi zote yaani TAIFA, JIMBO, SECTION, IDARA NA KANISA LA MAHALI PAMOJA zifanye ibada ya Kumshukuru na kumuomba Mungu hadi hapa tulipofikia IKIWA Ni pamoja na kusoma(bonyeza link hii) ZABURI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD
IKIAMBATANA NA KELELE ZA SIFA NA KUMUADHIMISHA MUNGU


Hawa ni viongozi na Wamishonari wa TAG wakisoma Zaburi ya Jubilee ya miaka 75 ya TAG MBELE ZA MUNGU katika uzinduzi wa sherehe za Jubilee tar 18 Jan 2014 pale Malizi Mbeya


Baadhi ya viongozi wa TAG wakipunga vitambaa kumuadhimisha Mungu kwa Miaka 75 ya TAG

Ukisoma kitabu cha Kumb 16:1-17 anazungumza kuhusu WanaIsrael kufanya sherehe za Maadhimisho
  1. Sherehe za Mikate isiyochachwa - Leo kwetu tunasherekea PASAKA
  2. Sherehe ya Majuma/mavuno - Leo tunasherekea SIKU YA PENTEKOSTE
  3. Sherehe ya Vibanda/kusafiri miaka 40 Jangwani - HAPA NDIPO PANAPOTUFANYA tusherekee maadhimisho mbalimbali, mfano familia wanaweza kumshukuru Mungu kwa miaka 20 ktk ndoa, Mkristo anaweza kumshukuru Mungu kwa miaka 10 tangu aokoke nk
Sisi Tanzania Assemblies of God ni safari ndefu tuliyo safiri tangu miaka ya 1939 KWA MIAKA 75 HATUNABUDI KUINUA MIKONO YETU NA KUMPA SIFA NA SHUKRANI MUNGU.
UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG  PALE MBALIZI MBEYA

UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG  PALE MBALIZI MBEYA

UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG  PALE MBALIZI MBEYA

UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG  PALE MBALIZI MBEYA






UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG UZINDUZI WA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TAG Reviewed by Unknown on 3:58 PM Rating: 5

No comments:

ads
Powered by Blogger.